The House of Favourite Newspapers

Rais wa Brazil Afungwa Jela kwa Kula Rushwa

0
Luiz Ignacio Lula da Silva

 

Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Ignacio Lula da Silva (71), amehukumiwa kifungo cha miaka tisa na nusu jela kutokana  na kupatikana na makossa ya rushwa yaliyokuwa yakimkabili.

Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha muungano, alijizolea umaarufu kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kuboresha maisha nchini Brazil.

Lakini sasa mambo yamegeuka na amekutwa na hatia ya kupokea rushwa ya zaidi  ya Sh. 2.5 bilioni za malipo ya  ukarabati wa ghorofa  lake la mapumziko kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, ya OAS.

Hukumu hii inakuja wakati Lula ameshatoa msimamo mkali kwamba, ana mpango wa kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea urais mwakani.

Kufuatia hukumu hiyo, Rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili wanaomtetea wakiahidi kukata rufaa.

Wakati huohuo, kamati ya Bunge la Congress ya Brazil inajadili iwapo iiruhusu mahakama kuu kusikiliza kesi ya rushwa inayomhusisha Rais mwingine wa Brazil Michel Temer.

Temer kwa upande wake, alishtakiwa mwezi uliopita kwa tuhuma za kupokea hongo kutoka kampuni kubwa ya usindikaji nyama.

Kamati hiyo inatarajiwa kupiga kura kesho.

Leave A Reply