Rais wa Guinea-Bissau Alivyotembelea Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR

Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, ametembelea mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR kati ya Dar es Salaam – Morogoro ambapo anatakwa kuwa ndiye Rais wa kwanza kutoka nje ya Nchi kuutembelea mradi huo na amesafiri na treni hiyo ku kutoka Dar es salaam mpaka Pugu.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbara amempokea Rais Embalo na ujumbe wake ambapo amesema Rais Embalo amefurahishwa sana na hatua kubwa ambayo Taifa la Tanzania limepiga kwenye miundombinu ya Reli ya Kisasa.

Reli ya SGR Kipande cha kwanza mpaka cha saba kutoka Dar mpaka Mwanza mpaka Kigoma kisha Msongati-Gitege, Burundi ikikamilika itapelekea Tanzania kuwa na kilometa takribani 2,300 na kuwa Nchi ya tatu Duniani kwa kujenga Reli ndefu zaidi duniani na kuwa Nchi ya kwanza kwa Nchi zinazoendelea.