The House of Favourite Newspapers

Rais Wa Hungary Ajiuzulu Baada Ya Kumsamehe Mwanamume Aliyekutwa Na Hatia

0

Rais wa Hungary, Katalin Novak amejiuzulu kutokana na ghadhabu ya raia baada ya kumsamehe mwanamume aliyekutwa na hatia katika kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto.

Rais Katalin  alikuwa anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kwa sababu ya uamuzi wake wenye utata wa kumsamehe mwanamume ambaye alipatikana na hatia ya kuficha uhalifu uliofanywa na mnyanyasaji wa kingono katika nyumba ya watoto.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 ametangaza katika ujumbe wa televisheni Jumamosi 10 Februari 2024 kwamba amejiuzulu wadhifa wake wa urais, baada ya kukaa madarakani tangu mwaka wa 2022.

Novak alikuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushika wadhifa wa Urais nchini Hungary.

HAWA wa DIAMOND ANA HALI MBAYA – MAMA YAKE ALIA KWA UCHUNGU – MWENYEWE AZUNGUMZA – ”SIPO SAWA”….

Leave A Reply