Rais Wa Indonesia Afanya Ziara Ikulu Ya Dar, Miradi Mikubwa Yasainiwa (Picha +Video)
Rais Samia Suluhu Hassan amemkaribisha Rais wa Indonesia, Joko Widodo katika Ikulu ya Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya Kikazi ya siku mbili Nchini, Agosti 22, 2023
Ziara ya Rais Widodo ni ya pili kwa Kiongozi wa Taifa la Indonesia aliyepo madarakani kutembelea Nchini
Tanzania na Indonesia zilianzisha uhusiano wa Kidiplomasia mwaka 1964, ambapo Indonesia ilifungua Ubalozi wake Tanzania