Rais Wa Namibia Atembelea Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Alakiwa Na Mkuu Wa Chuo Dkt Kikwete
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Namibia NetumboNandi-Ndaitwah alipowasili chuoni hapo leo asubuhi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kiserikali ya siku mbili nchini.
Rais Dkt. Nandi-Ndaitwah amefurahi kualikwa kuzungumza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo na ameeleza kuwa atatumia fursa hiyo kuwahamasisha wanafunzi kushiriki katika fursa mbalimbali za kujenga nchi kizalebdo na za uongozi.