The House of Favourite Newspapers

Rais Wa Rwanda Paul Kagame Amewasili Nchini Na Kupokelewa Na Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dares Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye Gadi ya Jeshi ya heshma pamoja na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili (hazionekani pichani ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kumpokea mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia frame ya Picha ya Kiasili aliyokabidhiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amewasili  nchini leo Jumapili, Januari 14 kwa ziara ya siku moja.

Rais Kagame aliyepokewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli,  baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere (JNIA) alielekea katika chumba maalum na kukaa kwa takribani dakika 30.

Aliondoka uwanjani hapo saa 4:47 asubuhi kuelekea Ikulu ambako atafanya mazungumzo na Rais Magufuli.

Hii ni mara ya pili kwa rais huyo kutembelea Tanzania tangu mwaka 2015,  mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2016 ambako alishiriki maonyesho ya 40 ya kimataifa ya biashara (sabasaba)

Comments are closed.