The House of Favourite Newspapers

Rais Paul Kagame Awasili Nchini Kwa Ziara ya Kikazi ya siku Mbili – (Picha +Video)

0

Rais wa Jamhuri ya Rwanda leo Aprili 27, 2023 amewasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Rais Kagame amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax.

Akiwa katika uwanja huo wa ndege, Rais Kagame amepata fursa ya kuangalia vikundi mbalimbali.vya burudani

Akiwa nchini pamoja na mambo mengine, Rais Kagame atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam.

Katika mapokezi hayo Dkt. Tax aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar Jamal Kassim Ali, Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Rwanda Nchini, Meja Jenerali Charles Karamba na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.

 

Leave A Reply