The House of Favourite Newspapers

Rais wa Rwanda, Paul Kagame Kuanza Ziara ya Siku Mbili Nchini

0

Rais wa Rwanda, Paul Kagame anatarajiwa kufanya ziara yakikazi nchini Tanzania kuanzia kesho, April 27 hadi April 28.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeeleza kuwa Kagame na ujumbe wake wanatarajiwa kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Waziri Stergomena Tax.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa akiwa nchini, Rais Kagame atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan ambapo baadaye, watazungumza na waandishi wa habari.

Leave A Reply