Kartra

Rais wa Uefa Akiri Mapungufu Euro 2020

 

ZIKIWA  zimesalia saa chache tu kabla ya ile fainali inayosubiriwa ya Euro 2020, Rais wa Shirikisho Soka la  Ulaya, Aleksander Ceferin anasema kuwa, hawatafanya makosa ya kurudia fomati ya mechi tena.

 

Katika mazungumzo na kipindi kimoja cha televishen, Ceferin anasema kuwa michuano ya mwaka huu imekuwa na mapungufu makubwa hasa kutokuwa na usawa, Hii inatokana na ukweli kuwa baadhi ya timu zinalazimika kusafiri mbali zaidi ya nyingine.

 

Katika michuano ya Euro 2020, kulikuwa na zaidi ya miji 11 ambayo ilikuwa ikishuhudia timu zaidi ya 24 zikigombania nafasi ya kuwa bingwa wa nchi za ulaya na mpaka sasa ni mbili tu zipo fainali.

 

Timu hizo mbili ni Uingereza na Italia ambapo fainali yake itapigwa leo saa 4:00 usiku katika Dimba la Wembley.


Toa comment