The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Rais wa Uganda Atangaza Kuachana na Mtandao wa X

0
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametangaza kuachana na Mtandao wa X

Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametangaza kuachana na Mtandao wa X (zamani Twitter) ambao amekuwa akiutumia kuchapisha jumbe zenye utata.

Jenerali huyo wa jeshi mwenye umri wa miaka 50, ameingia katika ulingo wa kisiasa, na kukiuka itifaki za kijeshi, na hivyo kuzua mijadala kuhusu azma yake ya kumrithi baba yake ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Hivi karibuni, alizusha hasira kwa ujumbe wa Twitter ambapo alitishia kumkata kichwa kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Bobi Wine.

Katika chapisho lake la mwisho siku ya Ijumaa, Jenerali Kainerugaba amesema:

“Wakati umefika sasa wa kuondoka na kuzingatia” majukumu yake ya kijeshi lakini akaahidi “kukutana tena” na wafuasi wake milioni moja katika siku zijazo.

Hii si mara ya kwanza kwa Jenerali Kainerugaba kuzima akaunti yake ya X. Mwaka 2022, aliacha mtandao huo na kisha kurudi siku chache baadaye.

DK SLAA AMPASUA MBOWE HADHARANI – ASEMA CHADEMA INAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA -MBOWE VS LISSU

Leave A Reply