The House of Favourite Newspapers

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson Alivyofunga Mkutano Jijini New York

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, akifungua Mkutano wa uwasilishaji wa maazimio ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, Februari 14,  2025, amefungua Mkutano wa uwasilishaji wa maazimio ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kuhusu taarifa za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) na hatua zilizopigwa na Mabunge Wanachama.

Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Trusteeship, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), Jijini New York, Marekani.

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za IPU kwa kushirikiana na UN kuhakikisha Mabunge yanatekeleza kikamilifu ajenda za maendeleo endelevu kupitia mijadala yenye tija, tathmini ya mafanikio na kushirikishana mbinu bora za utekelezaji.