Rais wa Urusi, Vladimir Putin Awasili nchini Mongolia kwa ziara
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amewasili nchini Mongolia kwa ziara rasmi, ikiwa ni mara ya kwanza kutembelea nchi hiyo tangu mwaka 2023.
Ziara hii imekuja wakati ambapo Mongolia imetia saini mkataba wa Roma unaotambua mamlaka ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ambayo imetoa hati ya kukamatwa kwa Putin kutokana na tuhuma za uhalifu wa kivita wakati wa uvamizi wa Ukraine.
Putin alifika katika mji mkuu wa Mongolia, Ulaanbaatar, Jumatatu jioni akikaribishwa kwa sherehe za zulia jekundu. Ziara hiyo inafanyika kwa mwaliko wa Rais wa Mongolia, Ukhnaagiin Khurelsukh ambaye alitoa pendekezo hilo wakati wa mkutano huko Beijing mwishoni mwa mwaka 2023, kama ilivyoripotiwa na shirika la habari la TASS.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuwasili kwa Putin, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine, Georgy Tikhyi, alikosoa vikali uamuzi wa Mongolia wa kutomkamata Putin kwa kibali cha ICC.
Dmitry Peskov alisisitiza kwamba Moscow haihofii kukamatwa kwa Putin nchini Mongolia chini ya kibali cha ICC, akisema, “Hakuna tatizo kama hilo na Mongolia,” kama alivyonukuliwa na TASS.