Rais wa Zamani Comoro Aomba Msaada Tanzania

Rais wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah Sambi hivi karibuni alimuandikia barua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambayo iliwekwa hadharani. Barua hiyo iligonga vichwa vya habari kwenye gazeti moja la kila siku la nchini Tanzania siku ya Jumanne wiki hii.

 

Kiongozi huyo wa zamani wa Comoro, anayezuiliwa nyumbani kwake tangu mwaka 2018, anasema anasikitishwa na kitendo cha kutofuatwa kwa sheria katika matibabu anayofanyiwa na anaomba msaada kutoka kwa Tanzania, kwa sababu madaktari wake wanaendelea kupendekeza aweze kupata matibabu zaidi huku wakimfuatilia kwa karibu.

 

Sehemu nyingi za barua hii zilionekana kwenye nakala hiyo. “Tafadhali nisaidie kurejesha uhuru wangu ambapo afya yangu inadhoofika. Haya ni aina ya maombi yaliyotolewa na rais wa zamani wa comoro Ahmed Abdallah Sambi katika barua aliyomuandikia mkuu wa nchi wa Tanzania. Wakili wake anathibitisha kuwa barua hii ilitumwa kwa Samia Suluhu Hassan mwezi uliopita.

 

Tayari Januari 2020, kulikuwa na mazungumzo ya rais huyo wa zamani kuachiliwa kwa sababu za kiafya na ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ilithibitisha kumuunga mkono. Kulingana na familia ya Bw. Sambi, barua hii ilikusudiwa kukumbusha nchi hii rafiki ambayo serikali ya Comoro inapuuza maombi yote yanayomhusu rais huyo wa zamani anayezuiliwa tangu mwezi Agosti 2018.

 

Hayo yanajiri wakati sheria ya Comoro inabaini kwamba mtu ana haki ya kuzuiliwa kwa muda ya miezi minane ikiwa kesi yake itakuwa bado haijakamilika.

 

Katika barua yake kwa rais, mfungwa huyo anaeleza kuwa yeye ni raia zaidi ya yote, baba ambaye hajawaona watoto wake kwa miaka mingi na ambaye haki zake za msingi zinakiukwa. Ahmed Abdallah Sambi anakariri kuwa afya yake inaendelea kuzorota na kwamba amefungwa kwa sababu za kisiasa. Anasema, kanuni yenyewe ya haki za binadamu haiheshimiwi.


Toa comment