The House of Favourite Newspapers
gunners X

Rais wa Zanzibar Dkt Mwinyi Akutana na Jumuiya ya Wahindu

0
Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa Jumuiya ya Wahindu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Mei 28, 2022 amekutana na Jumuiya ya Wahindu Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Arvind Asalwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 ya kukutana na makundi mbalimbali ili kubaini na kutafuta suluhu ya changamoto zinazowakabili.

 

Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali inahitaji Wawekezaji nchini kupitia sekta mbalimbali, hususan ile ya Uchumi wa Buluu, Usafirishaji pamoja na Biashara kupitia bahari huku akiwahakikishia wawekezaji hao ulinzi wa Rasilimali zao.

Aliongezea kusema:

Rais wa Zanzibar Dkt Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya Wahindu

“Kinachohitajika hivi sasa ni wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya haraka nchini”

 

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahindu Bwana Arvind Asawla alimshukuru Mhe. Rais Mwinyi kwa kusimamia vema ukusanyaji na matumizi ya Fedha za Serikali pamoja na kuleta maendeleo ya haraka Zanzibar.

Leave A Reply