Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi Alivyoondoka Zanzibar Kuja Jijini Dar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Jijini Dar es Salaam kushiriki dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa heshima ya mgeni wake Rais wa Poland, Andrzej Duda.
Rais wa Poland Mhe.Andrzej Duda amewasili kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini.