The House of Favourite Newspapers

Rais Weah Atangaza Kufuta Ada Vyuo Vikuu Vyote

Image result for George Weah
Rais George.

RAIS wa Liberia, George Weah, ametangaza Chuo Kikuu cha Liberia na vyuo vikuu vyote vya umma vitatoa mafunzo bure kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Ametangaza hivyo mbele ya mamia ya wanafunzi waliokuwa wakishangilia uamuzi huo jana (Jumatano) kwenye eneo la chuo hicho liitwalo  Capitol Hill Campus jijini  Monrovia katika ziara aliyofanya hapo.

Kwa mujibu wa gazeti la The African Exponent.  uamuzi wa kiongozi huyo aliyewahi kuwa nyota wa soka duniani, ni kuifanya Liberia kuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengine ya Afrika.

Uamuzi huo unafuatia maandamano yaliyosababishwa na kupandishwa kwa ada za chuo hicho kutoka Dola 4 za Marekani (sawa na Dola 400 za Liberia) kwa saa hadi kufikia Dola 600 za Liberia.

Wanafunzi hao walikuwa wamepinga kutofuatwa kwa sera ya chuo kikuu hicho ambayo inasema ongezeko la ada lisifanywe na upande mmoja, bali lishirikishe bodi ya wadhamini, bodi ya vitivo, uongozi wa wanafunzi na Rais wa Liberia.

Image result for George Weah

 

Rais aliuita uongozi wa chuo hicho wiki iliyopita baada ya kukutana na wanafunzi hao na hatimaye kuamua kufanya ziara chuoni hapo.  Uongozi wa chuo hicho ulikuwa umesema kwamba ongezeko hilo halikuwa la ada bali  ni ongezeko la viwango vya fedha dhidi ya Dola ya Marekani ambayo wanafunzi walikuwa wanaitumia katika malipo.

 

Chuo Kikuu cha Liberia kimeandikisha idadi ndogo ya wanafunzi msimu huu wa masomo ambayo ni wanafunzi 11,000 tu kati ya wanaokadiriwa kuwa 20,000.

Comments are closed.