Raja Casablanca Yatwaa Kombe la Shirikisho
KLABUya Raja Casablanca ya nchini Morocco, imetwaa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria usiku wa kuamkia leo huko jijini Cotonou nchini Cameroon.
Mabao ya Raja yalifungwa na washambuliaji wake, Soufiane Rahimi dakika ya 5 na Mkongomani Ben Malango Ngita dakika ya 14, kabla ya Mohammed Zakaria Boulahia kuifungia Kabylie bao la kufutia machozi dakika ya 46.
Baada ya Shirikisho sasa, Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itafuatia Jumamosi ijayo ambayo itazikutanisha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri kwenye Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca, Morocco.
Stori: Sifael Paul