Rally Bwalya Azungumza kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kutua Amazulu FC ya Sauz

KIUNGO aliyedumu akiwa na uzi wa Simba kwa miaka miwili, raia wa Zambia, Rally Bwalya, amesema kuwa kucheza kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini na klabu ya Amazulu FC ni kutimiza ndoto ambayo alikuwa nayo muda mrefu.

 

Bwalya alisema kuwa Amazulu ni moja kati ya timu kubwa Afrika Kusini na anaamini itakuwa sehemu ya yeye kuelekea kukua zaidi kisoka na kuipa mafanikio klabu hiyo na yeye kupata mafanikio binafsi.

 

“Kujiunga na Amazulu kwangu ni mafanikio makubwa kwani nimekuwa nikiitazama na kuifuatilia kwa muda mrefu Amazulu inajulikana sana kwetu Zambia kwa sababu watu wengi wanatazama PSL.

 

“Ni timu ambayo siyo mpya kwangu, jambo kubwa ni kuisaidia klabu yangu kwa jitihada zote kwani kila mchezaji anakuwa na malengo yake na kuisaidia klabu kufikia malengo yaliyowekwa kwa msimu husika,” alisema.

Bwalya aliagwa wiki iliyopita na Simba na amesaini mkataba wa miaka miwili kukipiga kwenye timu hiyo kutoka katika Mji wa Durban.3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment