The House of Favourite Newspapers

Ramadhan Brothers Waibuka Washindi Shindano la America’s Got Talent (AGT)

Wanamichezo wawili kutoka Tanzania maarufu kama Ramadhan Brothers wamefanikiwa kuibuka Washindi wa Shindano la Kusaka Vipaji la America’s Got Talent (AGT) na kuondoka na Dola za Marekani 250,000 (Takriban Tsh. Milioni 637.5)

Kundi hilo linaloundwa na Wanamichezo wa Sarakasi ambao ni Fadhili Ramadhani and Ibrahim Jobu walikuwa upande wa Jaji Howie Mandel, wamewashinda washiriki wengine ambao ni The Pack Drumline, V.Unbeatable, Sainted na Musa Motha

Ramadhani Brothers wanakuwa Watanzania wa kwanza kufanikiwa kushinda Mashindano ya “AGT”. Wakizungumza baada ya kutangazwa Washindi, wamesema Fedha hizo wataziwekeza katika Vifaa vya Mazoezi Nchini Tanzania.