Kartra

Ramos: Messi Anaweza Kuishi Kwangu

BEKI wa Paris Saint-Germain, Sergio Ramos amemwambia mchezaji mpya wa klabu hiyo, Lionel Messi anaweza kwenda kuishi nyumbani kwake yeye na familia kama atakuwa amechoka kuwa hotelini katika kipindi hiki ambacho bado anaweka mambo yake sawa.

 

”Kama wewe na familia yako mnapendelea kukaa nyumbani badala ya hotelini, mnaweza kuja kuishi kwangu,” kauli ya beki huyo wa miaka 35.

 

Messi na familia yake kwa sasa wanaishi, hotel Le Royal Monceau wakati akikamilisha mambo yake akiwa bado hajahamia katika makazi mengine hapo Ufaransa na kuanza kuwatumikia waajiri wake wapya PSG.

 

Sergio Ramos amekuwa mshindani mkubwa wa Messi kwa miaka mingi wawili hao walivyokuwa LaLiga, Hispania wakati mtukutu Ramos akiitumikia Real Madrid na Messi akiwa Barcelona lakini kwa sasa wamejikuta wakiwa wamesajiliwa kwenye klabu moja PSG


Toa comment