Rashford na casemiro walikubali tizi la amorim
Wachezaji wa Manchester united Marcus Rashford (27) pamoja na Carlos Henrique ‘Casemiro'( 32), wameonyesha kufurahishwa na mazoezi ya mkufunzi mpya wa klabu hiyo Ruben Amorim.
Marcus Rashford pamoja na Casemiro, walituma machapisho kwenye mitandao yao ya kijamii wakionyesha kukubaliana na hatua za mwanzo za mazoezi kutoka kwa mreno huyo.
Casemiro alichapisha kupitia ukurasa wake wa X akisema “Top training” akimaanisha mazoezi ya juu, wakati Rashford yeye alichapisha katika upande wake wa Instagram story akisema ”Top session today” akimaanisha kipindi bora leo.
Ruben Amorim ameanza kazi rasmi ya kuinoa klabu ya Manchester United, akichukua nafasi ya Erik Ten Haag aliyetimuliwa baada ya mwenendo mbovu wa klabu hiyo.
Ruben Amorim ataanza kibarua chake dhidi ya Ipswich town Jumapili ya wiki hii, ikiwa ni mchezo wa 12 msimu huu. Huku Manchester United wakiwa nafasi ya 13 na alama 15 katika michezo 11 ya ligi kuu ya Uingereza.