Rasmi: Dean Smith Kocha Mpya Norwich City

Klabu ya Norwich City imemteua Dean Smith kuwa kocha mpya wa kikosi hicho baada ya kumtimua Daniel Farke Novemba 7 mwaka huu. Smith amesaini kandarasi ya miaka miwili na nusu na atasaidia na Craig Shakespeare kama kocha msaidizi.

 

Smith ambae amefungashiwa virago kutoka Aston Villa, aliisaidia timu hiyo kupanda Ligi Kuu EPL, ndani ya msimu wake wa kwanza kabla ya kufuatiwa na misimu miwili ya mafanikio ndani ya EPL.

 

Smith kwa uzoefu wake vile vile aliisaidia Villa kufika Fainali ya kombe la Ligi msimu wa 2019/2020 lakini walipoteza mbele ya City katika uwanja wa Wembley.

 

Norwich kwa sasa inakamata nafasi ya mwisho katika msimamo wa EPL ikiwa na alama tano baada ya michezo 11. Je, Smith ataiepusha Norwich na janga la kushuka daraja mwishoni mwa msimu?2178
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment