The House of Favourite Newspapers

ads

Rasmi: Gabriel Jesus na Alex Telles Nje Fainali za Kombe la Dunia Nchini Qatar

0
Nyota wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Arsenal, Gabriel Jesus

NYOTA wa Klabu ya Arsenal na Timu ya Taifa ya Brazil Gabriel Jesus atakosekana katika mashindano ya fainali za kombe la dunia nchini Qatar kufuatia kuumia goti.

 

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na jarida la geglobo nyota huyo alipata majeraha ya goti katika mchezo dhidi ya Cameroon na baada ya vipimo imebainika kuwa atakaa nje muda mrefu.

Mlinzi wa kushoto wa Brazil, Alex Telles atakosekana Kombe la Dunia

Mchezaji mwingine ambaye anatarajiwa kuyakosa mashindano hayo ni mlinzi wa kushoto wa timu hiyo Alex Telles ambaye naye matatizo yake ya kiafya hayawezi kuimarika kwa siku za hivi karibuni.

 

Taarifa ya kuumia kwa Gabriel Jesus inakuja katika wakati mbaya ambao klabu yake ya Arsenal inahitaji huduma yake ili iweze kuendelea vyema na mbio za kuwania Kombe la Ligi Kuu nchini Uingereza ambalo halijawahi kuchukuliwa na klabu hiyo tangu ifanye hivyo mara ya mwisho miaka 18 iliyopita.

Leave A Reply