Kartra

Rasmi: Ramos Kutua PSG Leo

Aliyekuwa beki na nahodha wa Real Madrid ya Hispania Sergio Ramos huenda akafanyiwa vipimo vya afya baadae hii leo jijini Paris, Ufaransa.

 

Ramos atafanyiwa vipimo vya afya ikiwa ni sehemu ya kukamilisha mpango wa kusajiliwa na Klabu ya PSG. Taarifa za awali zinadai kuwa beki huyo kutoka Hispania atasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Klabu hiyo hadi Mwaka 2023.

 

Ramos ameondoka Real Madrid, kufuatia mkataba wake kufikia kikomo kwa wababe hao wa jiji la Madrid, huku akienguliwa kwenye mipango ya benchi la ufundi litakaloongozwa na Meneja kutoka Italia Carlo Ancelotti msimu ujao 2021/22.

 

Wakati huo huo taarifa kamili za Usajili wa Hakimi na Donnarumma katika Klabu ya PSG, huenda zikatolewa wakati wowote kuanzia leo.

 


Toa comment