The House of Favourite Newspapers

Rasmi: Sadio Mane Kuyakosa Mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia Qatar

0
Nyota wa Bayern Munich na Timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane atakosekana katika Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

NYOTA wa klabu ya Bayern Munich na Timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane atakosekana katika mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia zinazofanyika nchini Qatar mwaka 2022 kutokana na kufanyiwa upasuaji wa mguu wake alioumia wakati akiitumikia klabu hiyo ya Bundesliga.

 

Taarifa ya kutokuwepo kwenye mashindano hayo imethibitishwa na Chama cha Soka nchini Senegal ambapo awali kulikuwa na matumaini huenda nyota huyo angeweza kujumuishwa kwenye kikosi cha Senegal na kuweza kutoa mchango wake endapo kama angeweza kupona majeraha yake wakati mashindano hayo yakiwa yanaendelea.

Sadio Mane, nyota wa Timu ya Taifa ya Senegal

Klabu yake ya Bayern Munich nayo imethibitisha kuwa Mane (30) amefanikiwa kufanya upasuaji wake salama akiwa nchini Australia.

 

“Sadio Mane amefanikiwa kufanya upasuaji Innsbruck na Profesa Christian Fink pamoja na Dr. Andy Williams kutoka London, Uingereza siku ya alhamis Jioni. Imesema taarifa kutoka katika tovuti rasmi ya klabu hiyo.

 

Kocha Mkuu wa Senegal Alliou Cisse sasa atamtegemea mshambuliaji wa Watform Ismaila Sarr kama nyota wake wa kutegemewa katika kikosi cha timu hiyo chenye nyota wengine wengi kama Kalidou Koulibaly na Golikipa Edouard Mendy wa Chelsea ya nchini Uingereza.

Leave A Reply