The House of Favourite Newspapers
gunners X

RASTA ZA DIAMOND PLATNUMZ ZASHANGAZA

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz

MUONE-KANO mpya wa mwana-muziki Nasibu Abdul ‘Diamond PlatnumZ’ umezua gumzo, baada ya picha zake mbalimbali kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha amesuka nywele zake kwa mtindo wa Rasta.  

Baada ya picha hizo kusambaa, mashabaki wengi walifananisha muonekano huo na namna wanawake wanavyosuka, wengine wakifika mbali na kuandika komenti pia kwamba wanatamani staa huyo angekuwa ‘mwanaume tata’.

Kwa upande wa Diamond, akizungumzia muonekano huo alisema kwamba; Muonekano wangu ni hali ya kwenda na wakati tu na hakuna lolote lile la zaidi. “Lakini pia ikumbukwe kwamba kubadilika kimuonekano kwangu ni kawaida, nimebadilika sasa na nitaendelea kubadilika mara kwa mara!”

SHAMUMA AWADHI

Comments are closed.