RATIBA KAMILI MAZISHI YA DK MENGI -VIDEO

MWANASHERIA wa familia ya marehemu bilionea na aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi, Michael Ngalo, leo, Mei 4, 2019 ametoa ratiba ya mazishi ya kiongozi wake huyo.
Ngalo amesema mwili wa marehemu Mengi utawasilia saa 8:00 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Emirates.
Amesema baada ya hapo, mwili huo utapelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, siku hiyo ya Jumatatu na Jumanne utapelekwa kwenye viwanja vya Karimjee, Posta, jijini Dar kwa ajili ya kuagwa na wakazi wa Dar es Salaam na viunga vyake.
Baada ya kuagwa Karimjee, mwili huo utapelekwa nyumbani kwake, Ada-Estate, Kinondoni, jijini Dar hadi kesho yake Jumatano ambapo utapelekwa uwanja wa ndege tayari kwa kusafirishwa kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kisha kijijini kwake, Nkuu, Machame, kwa mazishi yatakayofanyika kesho yake, Alhamisi.


Comments are closed.