Kartra

Ratiba Ligi Ya Mabingwa Afrika 2021/22

SHIRIKISHO la mpira wa miguu barani Afrika (CAF), limetangaza ratiba ya kwanza ya mashindano ya vilabu barani Afrika kwa msimu wa 2021/2022. Mashindano yataanza rasmi kwa hatua ya awali mnamo Septemba 10, 2021.

 

Droo ya nani atakutana na nani katika raundi za awali itafanyika mnamo 15, Agosti 2021.

 

Dirisha la mataifa kuomba kuandaa fainali za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho litafunguliwa mnamo Novemba, 2021 huku katika michuano ya msimu wa 2021/22, Tanzania itawakilishwa na Azam FC na Biashara United kwenye Kombe la Shirikisho huku Simba SC na Yanga SC ikiingia kwenye Ligi ya Mabingwa 2021/22.


Toa comment