The House of Favourite Newspapers

Ratiba Ya Ligi Kuu Bara Imetoka, Ipo Hapa

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) limetangaza ratiba mpya ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19 itakayoanza Agosti 22 2018.

 

Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amesema ligi hiyo itahusisha jumla ya mechi 380 kutoka 240 ambazo zilikuwa zilichezwa msimu uliopita kutokana na ongezeko la timu.

 

Wambura ameeleza katika msimu wa 2017/18 ligi ilihusisha jumla ya timu 16 pekee lakini kuelekea msimu ujao kutakuwa na idadi ya timu 20 ambazo zimefanya kuwe na ongezeko la idadi ya mechi.

 

Ratiba hiyo inaonesha mechi zitakazoanza Agosti 22 ni baina ya Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons, Ruvu Shooting vsĀ  Ndanda FC, Singida United United dhidi ya Biashara FC, Alliance FC dhidi ya Mbao FC pamoja na Kagera Sugar watakaocheza na Mwadui FC.

 

Wakati huo mechi yenye msisimko mkubwa itakayowakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga, itachezwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo Simba atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.

Comments are closed.