Ratiba ya Ligi Ya Mabingwa Simba, Yanga Zapangiwa Timu

RATIBA ya awali ya Ligi ya Mabingwa imetoka ambapo wawakilishi wa Tazania Simba na Yanga wamezijua timu watakazoanza nazo.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wataanza kucheza na UD DO Sonso ya Msumbiji mchezo wa kwanza utachezwa kati ya Agosti 9/10/11 mwaka huu nchini Msumbiji huku ule wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23/24/25 jijini Dar.

Yanga itaanza kumenyana na Township rollers nchini Botswana na mchezo wa marudiano utapigwa Dar kisha mshindi wa mchezo huo atamenyana na mshindi kati ya Zesco na Green Mamba.


Loading...

Toa comment