Kartra

Ratiba ya Mazishi ya Zakaria Hans Poppe

Mwili wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu hiyo, Zakaria Hans Pope utaagwa kesho Jumatatu Septemba 13, 2021 katika ukumbi wa kalimjee Dar es Salaam.

Jumanne, Septemba 14, 2021 asubuhi familia kutoa heshima za mwisho nyumbani Ununio na mchana mwili wa marehemu kusafirishwa kwenda Iringa Mjini.

Mazishi yatafanyika Jumatano, Septemba 15, 2021 Kihesa Mkimbizi mkoani Iringa

Zakaria Hans PopeĀ  alifariki dunia jioni ya Ijumaa, Septemba 10, 2021 katika Hospitali ya Agha Khan alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.


Toa comment