Ray Afunguka Mrithi Chuchu Hans!

SIKU chache baada ya video inayomuonesha kaka mkubwa Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mrembo aliyefahamika kwa jina moja la Sarafina (Fina) kuvuja na kuzua maswali, hatimaye Ray ameibuka na kutoa maelezo yake.

 

Kwenye kipande hicho cha video kilichosambaa katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Ray alionekana akiwa ndani ya gari upande wa dereva huku Sarafina akiwa upande wa abiria, akichezea kifua chake kwa madaha huku kaka mkubwa, mkali wa sinema za Kibongo akisikika kwa mbalii akichombeza kwa sauti kama ya kimahaba hivi kisha wakacheka!

Kufuatia video hiyo, wananzengo wa mtandao huo walianza kuhoji maswali mbalimbali ikiwemo suala la Ray kummwaga mzazi mwenziye, Chuchu Hans na kubanjuka na kifaa hicho kipya.

 

“Mh! Kaka mkubwa naona kaamua kama noma na iwe noma, kaamua kujilipua. Sasa itakuwaje Chuchu? Wamemwagana jumla au? Au imevuja bila yeye kupenda? Halafu na Johari naye vipi walishaachana? Johari si ndiye anayefahamika hadi kwa mama Ray? Johari si alikuwa rafiki wa karibu wa Sarafina na ni msanii wao?” mtoa maoni mmoja alihoji mtandaoni.

 

Kufuatia ishu hiyo kutikisa mitandaoni, Risasi Jumamosi liliamua kumvutia waya Ray ili kumsikia anazungumziaje ishu hiyo ambapo alipopatikana alisema kuwa yeye siku zote hana muda wa kushindana na mtu yeyote kwenye mitandao na hakuna mtu asiyejua kazi yake ni muigizaji hivyo anawaacha waendelee kusema tu.

“Mimi nawaangalia tu watu wavyosema ovyo. Mara sijui nilikuwa na Tessy, mara Fina (Sarafina) sasa mimi nawaacha wenyewe watajua na kuhukumu wajuavyo naendelea na mambo yangu,” alisema Ray.

 

Aidha, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtamfuta Chuchu na kumuuliza anachukuliaje suala hilo la kudaiwa kunyang’anywa baba mtoto wake, ambapo alipopatikana alijibu kwa kifupi.

“Unajua kuna wakati mtu unaishiwa hata maneno ya kusema, halafu kingine sina muda tena wa kumfuatilia mtu na kama kaamua hivyo sawa ni kwa faida yake maana wengine tushazoea kuumizwa siku zote,” alisema Chuchu.

 

Kama hiyo haitoshi, Risasi Jumamosi limlimcheki Johari kwa njia ya simu na kumuuliza amelipokeaje suala hilo? Haya hapa majibu yake:

“Jamani watu wajue tu dunia inakaribia kufika mwisho na isitoshe huyo mwanamke (Sarafina) wanaosema alikuwa ni rafiki yangu wanakosea, rafiki yangu alikuwa ni marehemu mama yangu mzazi na si mtu mwingine yeyote,” alisema Johari.

 

TULIPOTOKA

Kabla ya clip hiyo kusambaa mitandaoni kuliwahi kuwa na tetesi kwamba Ray na Chuchu hawapiki na kupakua tena, madai ambayo hayajawahi kuthibitishwa.

Baadaye zilikuja tetesi nyingine kuwa, licha ya wawili hao kutokuwa kama zamani, Ray alipata kifaa kipya, mrembo aliyetajwa kwa jina la Tessy lakini haikuwahi kuthibitishwa hadi leo Ray alipomgusia kwenye stori hii wakati akizungumza na mwandishi wa Risasi Jumamosi.

 

Bado kuna utata kuhusu uhai wa penzi la Ray na Chuchu, lakini hata ukweli wa linalodaiwa penzi jipya kati ya Ray na Fina. Risasi Jumamosi bado linafuatilia na litakuletea mkanda mzima pindi utakapokamilika.

STORI: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi.


Loading...

Toa comment