The House of Favourite Newspapers

Ray C Amwandika Ruge: “Nibusu Shavuni, Vyovyote Vile, Nakupenda”

 

Mwanamuziki Rehema Chalamila maarufu kama ‘Ray C’ ameandika maneno yaliyowashangaza wengi huku yakiwaacha wengine vinywa wazi kwa ujumbe aliomwandikia Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Ruge Mutahaba  ambaye kwa wakati huu yupo nje ya nchi kwa matibabu.

 

Kupitia akaunti ya Ray C ya instagram ameandika: “Amka bwana, nashachoka kusubiri, msg zangu hujibu, simu hupokei, na stori kibao nataka kukwambia ingawa najua utanchamba lakini nishazoea kukwambia kila kitu changu kinachoendelea kwenye maisha yangu, tunagombanaga mpaka tunablokiana lakini tukionana tu tukaangaliana tunabaki kucheka tu.

 

Nishazoea kukwambia mambo yangu sababu we ndo msiri wangu, we ndo unanipaga makavu nikiharibu, Kuna muda mpaka nalia na ukiona nalia ndo unazidi kunipa makavu bila huruma.

 

Naondoka kwa hasira ingawa moyoni najua uliyoniambia ni kweli…. nakununiaaaaa ila haifiki wiki huyo nishakuja ofisini, Muda mwingine sina hata cha maana cha kukwambia ila nakuja tu ofisini kukuona unitanie nicheke!

 

Ray C umenimiss eeh…. Kama nywele hujazielewa unanipa live Ray nenda Katoe hizo nywele, Nikikuona tu napata amani ya moyo. Nikitoka tu studio wa kwanza kukutumia demo! ni wewe, wewe tu miaka yote tangu nimeanza muziki sababu naheshimu sikio lako na naliamini.

 

Mwezi wa ngapi sasa huu Ruge!Natuma msg, nakupigia, natamani kukuimbia japo kidogo upate nguvu sikupati..Ruge najua huko ulipo Unaumia sana,najua unataka kuamka na kufanya kazi zako. PLS WAKE UP babaa. Please!You are too strong babaa, Don’t give up Please..4 U

Nishike mkono, Nibusu shavuni, Vyovyote vile, Nakupenda. (Your favorite song )
#AmkaRuge,” ameandika Ray c

 

 

#ISIKUPITE :Msamaha wa Diamond kwa BASATA, MAPYA YAIBUKA!

 

Comments are closed.