RAY, KANUMBA WALIVYONOGESHA BONGO MUVI!

MIAKA ya 2010 na kuendelea, Bongo Muvi ndiyo ilishika kasi. Kama gari unaweza kusema ndiyo lilikuwa limewaka. Hiyo ni baada ya vijana wapiganaji, Vincent Kigosi ‘Ray’ na marehemu Steven Kanumba (Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) walikuwa wamea-chana na ulimw-engu wa maigizo na kuanza kuigiza filamu binafsi.

 

Wak-itokea katika Kundi la Kaole, walikuwa wames-hafanya filamu ya pamoja ya Johari chini ya Kampuni ya Game First Quality ambayo waliitoa mwaka 2007.

Kabla ya filamu hiyo, wengi tulikuwa tumewazoea kuwaona mastaa hao kupitia Runinga ya ITV katika michezo kama Fukuto, Baragumu, Jahazi na mingineyo.

 

Wakabadili mfumo wa sanaa kutoka ule wa michezo ya kwenye runinga hadi kuhifadhi kwenye mikanda ya V.H.S, upepo ukahamia huko na Watanzania wakawaelewa na kuwaunga mkono.

 

Wakazalisha mikanda mingi, wakazalisha na kusambaza kupitia kwa Kampuni ya Game First Quality (ya Mtitu), wakafanya ‘project’ nyingi chini ya mwamvuli wa Mtitu ambazo ziliwaongezea umaarufu hususan kutokana na jinsi walivyokuwa wakiigiza pamoja na kutengeneza pacha ya aina yake.

 

Si kwamba wakati huo hakukuwa na waigizaji wengine, walikuwepo wasanii wakubwa waliowazidi umri akina Ray na Kanumba akiwemo marehemu mzee Kipara, Dk Cheni, Bi Mwenda na wengineo ambao tayari walikuwa wakiigiza, lakini nyota tu iling’aa zaidi kwao.

 

Baada ya kuona wametengeneza umaarufu mkubwa kama vijana, walianza kujitanua. Ray kwa kushirikiana na mrembo Johari (Blandina Chagula) ambaye walikuwa na uhusiano wakaanzisha Kampuni ya RJ ikiwa imebeba kifupi cha majina yao (Ray na Johari).

 

Kampuni hiyo, Ray kama ‘kichwa’ aliifungulia nyumbani kwao maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar. Wakaajiri wafanyakazi, wakaanza kuzalisha sinema zao na kusambazwa na Kampuni ya Steps Entertainment ambayo wakati huo ndiyo ilikuwa ikinunua na kusambaza filamu za wasanii katika mfumo wa DVD.

 

KANUMBA ASOMA MCHEZO

Wakati huo Kanumba alibaki Mtitu Game akiendelea kuusoma mchezo ambapo aliweza kujitanua kwa kufanya filamu nyingi ikiwemo Dar to Lagos, Cross My Sin alizoshirikiana na nyota kutoka Nigeria akiwemo Mercy Johnson.

 

…AJIBU MAPIGO

Baada ya kuusoma mchezo akiwa chini Mtitu Game, Kanumba naye alimjibu Ray kwa kuanzisha kampuni yake ya Kanumba The Great Film na hapo ndipo vita ya wawili hao kisanaa iliposhika kasi.

Mashabiki wa sinema wakawa wanasikilizia kazi mpya kutoka kwa Ray kisha wanasikilizia kutoka kwa Kanumba naye atatoa nini.

 

…ANUNUA HIACE

Kanumba alinunua gari aina ya Toyota Hiace ya kufanyia shughuli za kuzalisha filamu aliyoipiga ‘machata’ ya The Great, Ray naye akajibu mapigo, akanunua Toyota Hiace aliyoiandika Ray The Greatest.

 

Mashabiki wao, mbali na kuvutiwa na majibizano yao katika upande wa sinema, bado walivutiwa na majibizano ya maisha yao binafsi hususan katika suala zima la maendeleo. Kama ingekuwa ni zama hizi tungeweza kusema kulikuwa na Team Ray na Team Kanumba.

 

RAY ATUNISHA MSULI

Ray kutaka kumuonesha Kanumba kwamba yeye ni kiboko, akanunua Toyota Land Cruiser V8 alilojinadi kuwa amenunua shilingi milioni 60, Kanumba naye akanunua Toyota Lexus alilojinasibu kuwa ni la shilingi milioni 78.

 

Hapo ilikuwa ni kazi baada ya kazi, mashabiki waliwafuatilia habari zao kuhusu kazi na maisha yao binafsi kupitia magazeti hususan ya Global Publishers ambayo yalikuwa yakichapisha habari zao mbalimbali.

 

Wakati moto wa ushindani ukizidi kushika kasi, Mungu alimchukua Kanumba ghafla mwaka 2012. Tangu hapo, Ray akapwaya katika ushindani. Akakosa pacha wa kuchuana naye. Kuna wakati Jacob Steven ‘JB’ alionekana kufiti, pia Gabo, lakini soko liliingiliwa na sinema za Kikorea na uharamia wa filamu, Bongo Muvi ikaonekana kupumulia mashine!

ERICK EVARIST

WOLPER – “Narudiana na HARMONIZE, Sarah Nilimuachia kwa Muda”

Loading...

Toa comment