Ray: Nazaa tena na Chuchu

MUIGIZAJI kitambo wa filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘ Ray’ amefunguka kuwa anataka kuzaa tena na muigizaji mwenzake, Chuchu Hansy mtoto mwingine.  Akipiga stori mbili tatu na Za Motomoto, Ray alisema kuwa ameona hakuna sababu ya kutafuta mwanamke mwingine wa kuzaa naye kwa sababu ni kuwatesa watoto hivyo Mungu akipenda yeye na Chuchu wataongeza mtoto mwingine hivi karibu.

“Unajua katika maisha lazima uchague kitu kimoja na kiwe cha kwako kabisa sasa mimi Chuchu ndiyo wangu na ndiye ambaye nitazaa naye mtoto wa pili,” alisema Ray aliyezaa naye mtoto mmoja, Jayden.

Stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment