Rayuu achefuliwa na wasanii wanaodandia waume za watu

rayuu skyna (2)Mrembo anayekimbiza kwenye soko la filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ hivi karibuni ametoa dukuduku la moyoni kwamba, anachukizwa na waigizaji wa kike ambao wamekuwa wakijitengenezea skendo za kutembea na waume za watu ili kutafuta umaarufu.

Akitoa dukuduku lake katika gazeti hili, Rayuu alisema msanii ambaye anajitambua na kujiheshimu, kamwe hawezi kufanya kitu kama hicho kwa kuwa atatambua kwamba yeye ni kioo cha jamii.

“Huwa nashangaa sana pale ninaposikia msanii fulani wa kike kakwaa skendo ya kuchepuka na mume wa mtu, sisi kama wasanii wa kike, tunatakiwa kujiheshimu, kama jamii imejitolea kukuheshimu kama msanii, kwa nini usijiheshimu? Skendo zipo ila hizi za kutembea na waume za watu zinashusha heshima, nadhani wengi wanatafuta kiki,” alisema Rayuu.


Loading...

Toa comment