The House of Favourite Newspapers

Rayvanny, Diamond, WCB Wapigwa Faini ya Tsh 9m na BASATA – Video

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limewatoza faini Tsh milioni 9 wanamuziki Rayvanny, Diamond Platnumz na Lebo yao ya WCB, kwa kutoa wimbo Mwanza ikieleza kuwa una mashairi yanayokiuka maadili.

 

Katibu wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza leo Novemba 13 katika ofisi za Baraza hilo zilizopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam, amesema Rayvany na Diamond kila mmoja atalipa faini ya Tsh milioni 3 na kwa Lebo ya WCB nayo italipa faini ya Tsh milioni 3 na kutakiwa kupeleka mashairi ya wimbo huo na kusisitiza kuwa hakuna mahala utakaporuhusiwa kupigwa hapa nchini Tanzania iwe usiku au mchana kwa kuwa hauifai.

 

Baada ya kufanyika kikao kati Rayvanny ambaye ndiye mwenye wimbo huo, kilichoketi kwa takribani saa tatu, Mngereza amesema;

“Huu wimbo haufai kabisa. Hata kwenye kikao tumemuuliza Rayvanny je, unaweza kuuimba mbele ya wazazi wako akajibu hapana, inaonyesha namna gani hata yeye anaona hauna maadili, na kwa nini tupige marufuku usipigwe halafu turuhusu ifanywe hivyo usiku?” alihoji Mngereza.

 

Meneja wa lebo ya Wasafi, Hamis Taletale ‘Babu Tale‘ amesema katika kikao yameamuliwa mambo mawili ikiwamo kupeleka mashairi ya wimbo huo yakahaririwe na kutoendelea kuusambaza.

 

Aidha, kuhusu kuufuta kwenye mitandao amesema hilo wataenda kulijibu kwa barua. Suala la wasanii wao kujitetea kupitia Instagram, amesema wameona mambo yatakayozungumzwa kikaoni huenda yakabaki humo, hivyo wameamua kutumia majukwaa ya mitandao kueleza utetezi wao.

RAYVANNY Alivyotinga BASATA leo kuwekwa Kikaangoni!

Comments are closed.