The House of Favourite Newspapers

Rayvanny: Mimi Ni Shabiki Mkubwa Wa Harmonize

0

MKALI wa ngoma ya Teamo, kutoka WCB, Rayvanny amefunguka kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa nyimbo za Harmonize licha ya kuwa msanii huyo hayupo kwenye lebo hiyo aliyodumu nayo kwa zaidi ya miaka kadhaa.

 

Rayvanny amesema hawezi kuitesa nafsi yake kwa kutopenda vitu vizuri, kwani Harmonize ni msanii aliyebarikiwa kipaji kikubwa na anafanya kazi nzuri licha ya kuwa kwa sasa hayupo tena WCB.

 

“Harmonize ni miongoni mwa wasanii wachache wenye vipaji vikubwa, aendelee kukazia hapohapo asiache kufanya kazi nzuri, kwa sababu nimeona albamu yake ni nzuri na amefanya kolabo na wasanii wakubwa Afrika,” alisema Rayvanny.

 

Baada ya kujitoa WCB, kwa sasa Harmonize anamiliki lebo yake ya Konde Music WorldWide na tayari ameshaachia albam ya Afro East yenye mikwaju 18.

Leave A Reply