MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi, leo Alhamisi, Agosti 30, 2018 ametembelea ofisi za makampuni ya Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam kisha kuzungumza na viongozi na wafanyakazi wa makampuni hayo.
Ofisi za Global Group zinajumuisha kampuni ya mbalimbali zikiwemo Global Digital na Global Publishers inayochapisha magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra.
Kiongozi huyo alipata fursa ya kuelezwa na viongozi wa kampuni na wa vitengo mbalimbali namna ambavyo kampuni hizo zimekuwa zikifanya kazi ikiwa ni pamoja na ukusanyaji na uandaaji wa habari, uandaaji wa gazeti (kusanifu kurasa) na usambazaji magazeti hayo kwenda kwa wasomaji.
Aidha, Hapi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, amepata fursa ya kuzungumza na waandishi na wahariri wa magazeti hayo ya Global Publishers ambayo kwa sasa yanaendesha promosheni kabambe ya Tusua Maisha na Global ambapo washindi wanajipatia zawadi za pikipiki, dinner set, ada za shule za watoto wao na jezi za soka kila wiki.
Kaima akimwonyesha Hapi magazeti yanayochapishwa na Global Publishers kwa wiki.
…Akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Amani ambalo huwa mitaani kila Alhamisi, Erick Evarist.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS
Comments are closed.