RC Awaita Watalaam wa Asili Kutibu Maradhi ya Kupumua

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema anawataka wale wote wenye tiba za asili za Pumu, Kifua, Mafua, Maumivu ya Mwili na Magonjwa yote yanayohusu Upumuaji.

 

Anawataka ofisini kwake ili wajitambulishe na kuonesha namna ambavyo dawa zao zinafanyakazi ili wasajiliwe na kusaidia tiba kwa maradhi ambayo yanayoendelea kuwataabisha watu nchini.

 

Mkuu wa Mkoa amesema uwepo wa watu wa Tiba za Asili ni fursa ambapo inaweza ikatatua tatizo lililopo na kuacha utegemezi wa fikra kwa dawa za wazungu.

Toa comment