The House of Favourite Newspapers

RC AYOUB AMSHUKURU JPM NA DKT SHEIN

0

 

 

Mkuu wa Mkoa wa mjini Magharibi, Zanzibar, Ayoub Mohammed Mahmoud, ametoa neno la shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein, viongozi wa serikali zote mbili, wananchi na waandishi wa habari kwa ujumla, kwa kuweza kufanikisha kumalizika kwa shughuli ya kuhitimisha kilele cha Mwenge wa Uhuru na maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere, ambazo zilifanyika Oktoba 14, katika uwanja wa Taifa wa Zanzibar wa Aman.

Aidha RC Ayoub, ameendelea kuwasisitiza wananchi wa mkoa wake kuendelea na harakati za kupingana vikali na vitendo viovu vinavyorudisha nyumba maendeleo ya mkoa wa Mjini Magharibi, vikiwemo vitendo vya rushwa, madawa ya kulevya, ukatili wa kijinsia, uhujumu wa uchumi wa nchi na vitendo vingine vyote visivyokubalika na jamii na vilivyokuwa kinyume na sheria ya nchi.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply