The House of Favourite Newspapers

RC Chalamila Atoa Maelekezo ya Kuzingatia Kuelekea Maandalizi ya Ujio wa Marais wa Afrika

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila Leo tarehe 11 Januari 2025 ameshiriki katika zoezi Maalumu la usafi wa Mji pamoja na Vyombo vya Usalama, Viongozi wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri na Taasisi za Umma lililofanyika katika Wilaya ya Ilala.

Akiwa katika zoezi Maalumu la Usafi RC Chalamila ametoa Maelekezo *Sita* ya kuzingatia kuelekea Maandalizi ya ujio wa Marais wa Afrika ikiwa ni pamoja na:-

Mosi, Eneo la feri linapaswa  kuwa safi ambapo Mhe. Chalamila amesema Soko Hilo kwa muda mrefu  limekuwa haliridhishi katika usafi hivyo kama atagundua bado hali ni mbaya tarehe 23- 25 atapafunga  na kuwaleta  Jeshi,  Polisi, Jkt, Zimamoto, Uhamiaji watafanya usafi mpaka pale watakapojifunza wafanyabiashara hao namna ya  kufanya biashara na kutunza mazingira

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameagiza Mchakato wa kumpata Mwekezaji Mkubwa wa Dampo uharakishwe mara Moja ili dampo lipate mwekezaji Mkubwa anayejitambua anayeweza kuzalisha ajira, gesi, na mbolea

Vile vile RC Chalamila ameongeza kuwa Barabara ya feri kwenda hyati, Johari Rotana   mpaka stesheni  itafungwa *kwa baadhi ya vyombo vya usafiri* na kuelekezwa vipite wapi  ili wageni wetu watakapokuwa hapa kusiwe na foleni kubwa

Aidhaa, Mhe. Mkuu wa Mkoa amemuagiza Katibu Tawala kuwasimamia  watendaji wote wa maeneo ya  kuanzia TPA kuja Temesa kuelekea Jiji kuwa yawe safi

Wakati huo huo RC Chalamila amesisitiza kuwa Barabara zitakazotumiwa na Marais kwa ajili ya mazoezi  ziwashwe taa ili vibaba wadogo wadogo waweze kuwa na aibu kutokana na taa zinazowaka

Mwisho Mhe.Chalamila akasisitiza kuwa kibaka wote kuanzia Leo atakayekamatwa apelekwe maabara ili kiwe chombo Cha kufundishia kwa wanafunzi wanaotaka kuja kuwa wezi (watakaojifunza kuwa wizi haustahili katika Jiji la Dar es Salaam).

 

Leave A Reply