RC Chalamila Atolea Ufafanuzi Changamoto Ya Bi. Martha Na Amana Hospitali – Video

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amekutana na kufanya mahojiano na Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Amana, watumishi Pamoja na Bi. Martha Lazi Mbele ya vyombo vya habari ikiwa ni katika kutatua changamoto ya madeni ya Bi Martha, pamoja na kulitolea ufafanuzi jambo Hilo.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa ameagiza uongozi wa Amana Hospitali kufanya uchunguza wa nyaraka na Viambatanisho muhimu kwa lengo la kujiridhisha kisha kukamilisha malipo yake kulingana na makubaliano ya Mkataba.
RC Chalamila ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salam, alipofika katika Hospitali ya Amana Baada ya Kusambaa kwa ‘Video Clip’ katika Mitandao ya Kijamii ikimuonesha Bi Martha akieleza kuidai Hospitali hiyo Fedha kama malipo Baaada kukamilisha Tenda ya ushonaji wa nguo Pamoja na mapazia katika Chumba cha Upasuaji.
Akieleza Mbele ya RC Chalamila, Bi. Martha alieleza kudai kiasi cha Zaidi ya Shilingi Milioni 5 kutokana na kazi hiyo ambayo aliifanya mnamo mwaka 2017 pamoja na mwaka 2021.
Pia, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Amana Dkt Bryceson Kiwelu ameeleza kupokea maagizo hayo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila kuhusu Suala la Bi Martha na kuahidi kuyatekeleza kwa uharaka zaidi ili kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amejitolea kumsaidia Bi. Martha kiasi cha shilingi Milioni 2 kwaajili ya kumsaidia katika kuendeleza shughuli zake za kijasiriamali