The House of Favourite Newspapers

LEYLA ALIYEUAWA UINGEREZA AZIKWA KWAO ARUSHA (Picha + Video)

Mwili wa marehemu Leyla ukipelekwa makaburini Sinoni kwa maziko.

 

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, jana ameongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya marehemu Leyla Mtumwa aliyeuawa na mumewe, Kema Kasambula, kwa kuchomwa visu mwezi uliopita jijini London nchini Uingereza.Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya Sinoni jijini Arusha.

 

Mwili wa Leyla uliokuwa ukishikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uingereza kwa ajili ya uchunguzi  ulikabidhiwa kwa familia yake na kuletea nchini Jumatatu.

 

Leyla anadaiwa kuuawa na mumewe huyo, usiku wa kuamkia Machi 30, mwaka huu jijini humo na sasa anakabiliwa na kesi ya mauaji.

Baadhi ya waombelezaji wakiomba dua baada ya maziko.

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati mwenye baraghashia) akiongea na waombolezaji baada ya maziko.
Kaburi la marehemu Leyla likiwekwa sawa baada ya maziko yaliyofanyika katika makaburi ya Sinoni jijini Arusha jana.
Mazishi yakiendelea.

(Habari na Korumba Moshi, Arusha)

RC Gambo Ampa Pole Hidaya Kwa Kufiwa na Mwanaye

HII NDIYO NYUMBA ALIMOUAWA LEYLA UINGEREZA

RIPOTI: Kifo cha Mtanzania Leyla Aliyeuawa UK, Mume Ahojiwa na Polisi!

Comments are closed.