RC Kilimanjaro Alivyoongoza Zoezi La Upandaji Miti Kwenye Kampeni Ya Tigo For Kili
Share
Mgeni rasimi kwenye kampeni ya tigo for kili Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mengeni Kitasha Wilaya ya Rombo, kwenye kampeni ya kuotesha miti katika Hifadhi ya Mlimakilimanjaro, iliyofanyika jana. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akiotesha mti katika eneo la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, lililopo Kijiji cha Mengeni Kitasha Wilaya ya Rombo, zoezi la upapandaji miti linafadhiliwa na tigo wakishirikiana na WWF. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akimwagilia maji kwenye mti alio uotesha jana katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kampeni ya kuhifadhi uoto wa asili katika mlima huo. Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raimond Mwangwala, akimwagilia maji kwenye mti alio uotesha jana katika kijiji cha Mengeni Kitasha Wilaya ya Rombo kwajili ya kutunza mazingiri kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.