The House of Favourite Newspapers

RC Kunenge Awashauri Wananchi Kupima Magonjwa Yasiyoambukiza.

0

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kujiwekea utaratibu wa kupima magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na saratani ya tezi dume, saratani ya matiti na mlango wa kizazi Kutokana na magonjwa hayo kusumbua wananchi wengi.

 

RC Kunenge ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 40 ya taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR).

Hata hivyo RC Kunenge amesema Kutokana na ukuaji wa teknolojia tezi dume sikuizi ni rahisi kupima kwa kutumia njia ya damu na mtu akapata majibu ya vipimo hivyo halina sababu yoyote ya watu kuwa na wasiwasi.

 

Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa taasisi ya NIMR kuendelea kufanya tafiti nyingi za tiba mbadala Kutokana na tiba hiyo kuonekana kufanya vizuri.

 

RC Kunenge amesema Taifa limebahatika kuwa na mimea ya kila aina hivyo anaamini tafiti za kutosha zikifanyika itasaidia kubuni dawa mbalimbali zitokanazo na mizizi, mimea na matunda na kusaidia wananchi.

 

Hata hivyo RC Kunenge amewashauri pia kufanya tafiti za tiba mbalimbali za magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, saratani, tatizo la moyo na Shinikizo la damu ambayo yamekuwa yakiwatesa wananchi wengi kwa Sasa.

 

Pamoja na hayo RC Kunenge ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.

Leave A Reply