The House of Favourite Newspapers

RC Makalla: Wakazi Dar Chukueni Tahadhari ya Covid-19

0

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewataka wakazi wa mkoa huo kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

 

Ametoa tahadhali hiyo leo Alhamisi Juni 24, 2021 baada ya Serikali kueleza tishio la mlipuko wa wimbi la tatu la ugonjwa huo katika nchi za Afrika zikiwemo nchi zinazopakana na Tanzania.

 

Akizungumza na wananchi leo Makalla amesema tahadhali ni muhimu kwa sababu kuna mwingiliano mkubwa kati ya mkoa huo na nchi jirani.

 

“Tahadhari hizo ni pamoja na kuvaa kwa usahihi barakoa kila wakati na sehemu zenye mikusanyiko na watu wengi kama kwenye vyombo vya usafiri wa nchi kavu na majini na vituo vyake, kwenye masoko, mikutano, sherehe, vituo vya kutolea huduma za afya, ofisini, baa na kwa wanafunzi darasani,” amesema.

 

Amesema hatua nyingine ni kunawa kwa maji tiririka mara kwa mara na kwa kutumia sabuni, kutosogeleana kwa karibu, kupaka vipukusi, kufunika mikono na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya kwa kutumia kiwiko cha mkono au kitambaa safi.

 

Makalla ameagiza katika maeneo ya taasisi mbalimbali na kwenye vituo vya usafiri wa majini na nchi kavu na maeneo yote yenye msongamano, wasimamizi wa maeneo yote wahakikishe wanaweka ndoo na miundombinu mingine ya maji tiririka.

Leave A Reply