The House of Favourite Newspapers

RC MAKONDA AKABIDHI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWENYE JIMBO LA KAWE.

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara kwenye Jimbo la Kawe kwa lengo la kukabidhi Miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwa Chama cha Mapinduzi CCM ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizozitoa Rais Dkt. John Magufuli kupitia ilani ya Chama hicho.

Miongoni mwa miradi aliyokabidhi RC Makonda ni Mradi Mkubwa kabisa wa Kuchakata taka wenye thamani ya Bilioni 5.59 uliopo Mwabwepande, Mradi wa Shule Mpya ya sekondari ya Mabwe Tumaini Girls iliyogharimu Shilingi Bilioni 2.6 na Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Kinondoni iliyopo Mabwepande yenye thamani ya Bilioni 2.4.

Akizunguza na Global publishers, RC Makonda amesama Chama Cha Mapinduzi kimetekeza Ilani na sasa wanakabidhi miradi hiyo.

“Mradi wa Matank makubwa matano na Pampu za kusambaza Maji zilizopo ambazo zipo Changanyikeni, Ujenzi wa Kituo cha Afya Bunju chenye thamani ya milioni 600, Mradi wa Makazi ya Askari Mabwepande pamoja na Zahanati ya Mkoroshini kata ya Msasani yenye thamani ya Milioni 408 hivi vyote navikabidhi ili Wananchi waliwachagua waone kazi kubwa iliyofanyika,”alisema.

Aidha katika ziara hiyo RC Makonda amewahimiza wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi watakaowaletea maendeleo na sio viongozi wanaopinga kila jambo jema linalofanywa na serikali.

Hata hivyo RC Makonda amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni outfits eneo kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya Kawe ili kusogeza huduma za Afya kwa wananchi wa kata hiyo.

Kesho RC Makonda ataendelea na ziara yake ya kukabidhi miradi kwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Jimbo la Kinondoni.

Leave A Reply