The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Akabidhi Milioni 38 Kwa Washindi Wa Samia Motocross Championship (Picha +Video)

0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda Julai 14, 2024 amekabidhi jumla ya fedha taslimu shilingi Milioni 38 za Kitanzania kwa washindi wa vipengele mbalimbali vya mashindano ya pikipiki ya Samia Motocross Championship.

Kelvin Gabriel ndiye aliyetangazwa kama mshindi wa jumla kwenye mashindano hayo akiondoka na fedha taslimu shilingi Milioni kumi za Kitanzania ambapo Mkuu wa Mkoa Makonda ameahidi pia kuwashika mkono kwenye kushiriki michuano ya kikanda na Kimataifa.

Msisimko mkubwa pia umekuwa kwa ndugu pacha Yannick Allad na Manuel Allard ambao wameibuka mshindi wa kwanza na wa pili kwenye kundi la Inter Midietly, wakikiri wazi kuwa baba yao mzazi amekuwa msaada mkubwa na mwalimu wao katika kukimbiza pikipiki.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda akimkabidhi mshindi wa tatu category ya Intermidiate Colin Simonson zawadi ya shilingi milioni mbili na medali baada ya kushinda mbio za Pikipiki SAMIA MOTOCRSS CHAMPIONSHIP .

Leave A Reply