The House of Favourite Newspapers

Makonda Amtaka Mkandarasi Kukamilisha Barabara Ya Sinza -Video

0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kwa mmoja wa wasimamizi wa barabara  hiyo.
Barabara ya Sinza inayoanzia Bamaga hadi Shekilango.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amemtaka Mkandarasi anayejenga Barabara ya Sinza inayoanzia Bamaga hadi Shekilango kuhakikisha Ujenzi unakamilika kwa Wakati ili kupunguza kilio cha foleni kwa watumiaji wa njia hiyo.

 

Makonda amesema barabara hiyo inayojengwa ina urefu wa Km 3.7 na upana wa Mita 22 ambapo itakuwa na Njia nne za Magari pamoja na Barabara ya watembea kwa miguu, Taa za Kisasa, Mitaro ya Maji na Bustani.

 

Aidha RC Makonda amesema ujenzi huo unaenda sambamba na ujenzi wa Barabara unganishi ikiwemo ya Kuelekea Kebbys hotel, Chuo cha ustawi wa jamii, Mwenge TRA, Sinza Mapambano, Lion hotel, Sinza meeda na Barabara ya Sinza Makaburini.

 

Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza Viongozi wote wa Mkoa, Wilaya na Jiji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi na kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliokusudiwa.

MAKONDA Atoa MUONGOZO wa ‘PARTY’ ya CORONA, “Kila Mtu Asherehekee kwa STAILI Yake”

Leave A Reply